TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI (NLUPC)

tume@gmail.com

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.
3 ya 1984 na badae ikafanyiwa marekebisho na Sheria Na. 6 ya 2007 (Sura 116). Kuanzishwa
kwa Tume kulionekana kuwa na umuhimu baada ya kubaini kuwa sera, sheria, na taasisi
iliyoundwa haikuwa na ufanisi wa kutosha katika kuratibu shughuli na programu mbalimbali
zinazohusiana na matunzi ya ardhi zinazofanywa na asasi mbalimbali za kisekta katika Serikali,
sekta binafsi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Tume ilianzishwa ili kuwianisha na kuratibu sera
na sheria zote zinazohusiana na matumizi ya ardhi, ili kukuza usimamizi bora na uboreshaji wa
ubora wa ardhi kwa lengo la kuhakikisha matumizi endelevu ya ardhi, ili iweze kutoa uzalishaji
bora ili kuimarisha kijamii na kiuchumi. Maendeleo ya kiuchumi na matengenezo ya ubora wa rdhi
kwa tija ya muda mrefu.

Our Latest Jobs

;