Afisa kilimo msaidizi

Kilimo Industry
Responsibilities

a) Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani
wa zao la korosho kwa kufanya yafuatayo:-
i. Kutoa elimu ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima kuanzia kuandaa shamba, kutunza
shamba, kuvuna, kuongeza thamani, kuhifadhi hadi kuuza sokoni.
ii. Kutoa elimu na kusimamia ubora wa korosho ghafi kuanzia shambani hadi ghalani.
iii. Kufuatilia na kuhakikisha kuwa wakulima wanazingatia Kanuni za kilimo bora cha korosho.
iv. Kuandaa na kutoa taarifa kila wiki kuhusu maendeleo ya kilimo cha korosho katika eneo
husika la kazi.
v. Kuandaa mahitaji halisi ya pembejeo ikiwa ni pamoja na mbegu/miche kwa wakulima na
kuwasilisha Bodi ya Korosho Tanzania.
vi. Kusimamia na kuhakikisha pembejeo zilizosambazwa katika eneo husika zinawafikia
wakulima na wanazitumia katika mashamba yao ya mikorosho.
b. Kuhuisha kanzidata ya wakulima wa korosho na wadau wengine ikiwemo watoa huduma za
pembejeo katika eneo lake kwenye mfumo wa kidijitali uliopo.
c. Kusimamia ugawaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho zinazotolewa na Serikali kwa
wakulima wa korosho katika eneo lake la kazi.
d. Kutoa mafunzo ya kilimo bora cha korosho ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi na salama ya
viuatilifu kwa wakulima.
e. Kusimamia uhakiki wa ubora wa korosho katika ngazi ya Chama cha Msingi cha Ushirika
(AMCOS).
f. Kuanzisha mashamba ya mfano na shamba darasa katika eneo la kazi.
g. Kuandaa makadirio ya uzalishaji wa korosho ghafi kwa kuzingatia kigezo cha miti ya mikorosho
iliyopo yenye uwezo wa kuzalisha katika msimu husika (Crop forecast).
h. Kukusanya taarifa/takwimu za korosho zinazobanguliwa majumbani/vikundi vidogo vya
ubanguaji na kuwasilisha Bodi ya Korosho Tanzania.
i. Kuwatambua wadau wa sekta ya kilimo waliopo katika eneo husika la kazi na kuwaunganisha
na wakulima ili kupata huduma wanazotoa.
j. Kuhakikisha kila mkulima ana daftari ambalo litatumika kujaza huduma
zitakazotolewa na wadau mbalimbali wakiwemo maafisa ugani kilimo.
k. Kushirikiana na uongozi wa kijiji kuchagua mkulima kiongozi (Lead farmer).
l. Kutoa ushauri kwa mazao mengine yanayolimwa na wakulima wa Kijiji/eneo
analosimamia.
m. Kufanya tathmini ya uzalishaji na ubanguaji wa korosho katika eneo lake la kazi kila mwisho

Qualifications

• Awe mtanzania mwaminifu, mwadilifu, mwenye kujituma na mahusiano mazuri na wengine.
• Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 35.
• Awe amehitimu stashahada (Diploma) katika fani ya sayansi ya kilimo (Agriculture General), agronomia (Agronomy), kilimo cha bustani (Horticulture) au uzalishaji wa mazao (Crop Production) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
• Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma.
• Awe hajawahi kufungwa kwa makosa yoyote ya jinai.
• Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini.
• Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa.
• Awe tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama itakavyoainishwa katika mkataba.
• Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa kipindi cha msimu husika.
• Uzoefu wa kazi katika zao la korosho ni sifa ya ziada.

Job Details


Kilimo
Kilimo na Rasilimali Asili
N/A
Contract
Huduma za Usaidizi wa Kilimo
400
1 Year
Monthly
No
  • Date Posted:
    20th Nov, 2024
  • Location:
    Dar es Salaam , Dar es Salaam, Tanzania
  • Expires On:
    2nd Dec, 2024
  • Job Skills:
    Awe mtanzania mwaminifu, mwadilifu, mwenye kujituma na mahusiano mazuri na wengine. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 35. Awe amehitimu stashahada (Diploma) katika fani ya s
Share This Job
Company Overview
CHUO KIKUU CHA SOKOINE
Tanzania
1 Open Jobs

Chuo kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kinashirikiana na Wizara ya Kilimo katika utekelezaji
wa programu ya kushirikisha vijana katika kilimo ya Jenga Kesho Iliyo bora (Building a Better
tomorrow- BBT). BBT inatekelezwa kupitia mikakati na miradi mbalimbali katika mnyororo wa
thamani wa mazao na baadhi ya malengo yake ni kuongeza ajira kwa vijana na wanawake
20,000 kupitia shughuli za kukuza ujuzi (internship), kuanzisha shughuli za kiuchumi 12,000
katika ngazi ya vijiji pamoja na kilimo cha mashamba makubwa (Block farms) ifikapo mwaka
2030. 

Related Jobs

;