I. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
II. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
III. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
IV. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
V. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
VI. Kufanya usafi wa gari; na
VII. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.