Nafasi za kazi Jeshi la Uhamiaji

Security Industry
Responsibilities

i. Awe ni raia wa Tanzania;
ii. Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;
iii. Awe na Cheti cha Kuzaliwa;
iv. Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
v. Awe na siha njema ya mwili na akili.
vi. Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;
vii. Asiwe na Kumbukumbu au Taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio
ya uhalifu au jinai;
viii. Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;
ix. Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;
x. Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na umri kuanzia miaka 18 hadi
miaka 22, Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Sita na Stashahada awe na
umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 25 na Mwombaji mwenye Elimu ya
Shahada/Stashahada ya Juu awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 30.
xi. Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.
xii. Awe tayari kujigharimia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la
Ajira.

Qualifications

Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma ngazi ya
Shahada/Stashahada ya Juu, Stashahada na Astashahada kutoka katika Vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali wenye fani zifuatazo:- Mtaalamu wa Lugha za Kimataifa,
Utawala, Sheria, Uhusiano, TEHAMA, Masijala, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi
na Ugavi waliosajiliwa na Bodi, Takwimu, Uchumi, Umeme, Ufundi wa Magari, Ufundi
wa AC, Cyber Security, Brass band, na Mpiga chapa (Printer).

Additional Information

i. Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika mfumo wa jpg/png isiyozidi
300Kb kwa ajili ya kuambatisha kwenye mfumo (upload);
ii. Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono;
iii. Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio
Makambini JKT/JKU wawe na barua za Utambulisho kutoka kwa Mkuu wa
Kambi;
iv. Cheti cha Kuzaliwa;
v. Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA kwa ajili ya kujisajili
kwenye mfumo;
vi. Awe na Index namba za vyeti vya kufaulu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita
ambazo atajaza kwenye mfumo wa ajira;
vii. Vyeti vingine vya kuhitimu fani mbalimbali ngazi ya Astashahada, Stashahada,
na Shahada/Stashahada ya Juu (kama anavyo na viwe vimehakikiwa katika
vyuo husika);
viii. Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi;
ix. Wasifu wa Mwombaji (CV).

Benefits

Job Details


Security
public sector
N/A
N/A
IT Support
1
1 Year
Monthly
No
  • Date Posted:
    4th Dec, 2024
  • Location:
    Dodoma , Dodoma, Tanzania
  • Expires On:
    31st Dec, 2024
  • Job Skills:
    Strong Communication
Share This Job

;